Nikuite jina gani hili nikuabudu
Hata kukuabudu vingine vipi ila nikupe sifa,
Na sifa nazo gani sababu yote majina
Yote ya sifa umekwisha kabidhiwa
Milele wakheri wametunga zako nyimbo za sifa
Alpha na Omega Mwikhulu Mungu Muumba watamukwa
Langu tu hata kama ni kama tone baharini
Furaha ninayohitimu nikijua Upo ni sifa dhabiti
Utukufu wako lugha zetu bina-Adamu zalemewa kitimiza umarufu
Uwezo wako watuacha mdomo wazi
Unalotaka toka kwetu kukuheshimu kukupenda kukuinamia
Hilo tu, twakamilisha tukipenda wenzetu
Sio kafara, sifa, wala maombi yatakayotuleta karibu nawe!
Ukaumba dunia nzima iweje kanisa mahala pa kukuabudu'
Ilhali roho zetu makao yako twachafua?
Ila sio penzi lako kwetu wakosefu binadamu kuhishi ndio hatustahili!
New beginnings
Wednesday, September 30, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment