New beginnings

Friday, April 9, 2010

BAADA YA IBADA BINADAMU DHAIFU

Mikono twashiikaba tukiimba zako sifa
Zetu roho kanisanai twakufungulia
Kabila, mila, rangi kando twaziweka
Sad to say this stops outside the gates of your holy house

Ukatuumba kwa mfano wako
Ukatuumba kwa umbo lako wewe uliye juu ya viumbe vyote
Yanihuzunisha twakugeuka tunapotendea wenzetu mabaya
Akili zetu ncha twajidanganya tunapofunga macho kwa mahitaji ya ndugu zetu

Mahali twakutani gani gari ghari dhibitisho la aliyehitimu
Viti vya mbele kanisana twapata kwa uwezo wa sadaka kutoa
Jameni ustadi wa mienendo usafi wa roho tena sio lengo la maana?
Kanisa kageuka kutoka Chumba cha kiroho kawa cha kifedha

Masikini kanisa la mabati enoe mitaa ya mabanda
Tajiri wakuabudu kwa nyumba za fahari sadaka ni dhahabu
Twasahau mjane aliyetoa tafaka ya juu ya centi pekee alokuwa nazo
Dhaifu mienendo yetu bina Adamu twakukera unayetupenda

Roho zetu kawa ngumu macho hayaoni wanaohitaji
Twasherehekea tukisahau wasojiweza
Shangwe zetu nafananisha na kicheko cha kifo, cha dharau
Ila tu utu ungekithiri dunia tungebadilisha ikawa mahala pema pa mwanadamu

Mbwa wapitanapo usalimiana
Hata kama kusimama kando na kunusana hata vita ni kuamkiana
Binadamu kununa ndio mtindo
Twakataa jukumu tulopewa la brother’s keeper.

Kiswahili is a challenging language I must say, but then we owe it upon ourselves to rise to the occasion now and then and do what need be done

3 comments:

  1. great i must say. kiswahili unakifahamu mwanangu

    ReplyDelete
  2. I had to get a kamusi for this!

    ReplyDelete
  3. Asanteni sana dada zangu! Mmenitia moyo wa kuendelea!

    ReplyDelete